Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.
HAKI YA KUSITIRIANA NA KUWEKEANA SIRI;
Haki ya mwisho tutakayo zungumzia katika nakala zetu hizi, ni haki ya mke kumsitiri mume wake, haki hii ni miongoni mwa zile haki ambazo zinawahusu wana ndoa wote wawili, kila mmoja anapaswa kumsitiri mwenzie, ama katika nakala hii tutazungumzia upande wa mke kwa kumsitiri mume wake na ni yepi yanayompasa kufanya ili kuhakikisha kweli amemsitiri mume wake.
Jambo la kwanza ni kwamba mwanamke yuapaswa kujiifadhi na kuweka siri za mume wake, iwapo kuna chochote ambacho mume wako amemjulisha, yanayowahusu wote wawili, au yanayomhusu mume pekee, iwe ni shughuli za kazini au yeyote ile, mwanamke huyo hapaswi kuyatangaza.
Jambo lingine ni kuwa, mke yuapaswa kuyaficha na kuyasitiri mapungufu ya mume wake ya siri, na hapaswi kuyatangaza inje au ata kwa watu wa karibu, kwani afahamu kuwa, kwa kudhalilika yeye ndo kudhalilika kwa mume wake, yale mapungufu ambayo atayataja kule inje, athari yake itarudi kwa wao wote wawili. Hasiwe ni mwenye kutangaza ata kwa watu wake wa karibu ambao anafahamu kuwa hawato msaidia kwa njia yeyote ile kinasaha zaidi ya kumuonea huruma na kumsema kwa wengine. Mke yuapaswa afahamu kuwa kwa kuyatangaza mapungufu ya siri za mume wake, atakua amemdhalilisha katika jamii na atakua amemuondolea heshima mume wake pale atakapo kuwa anatoka nje ya nyumba yake.
Mwenyezi Mungu (swt) anatuambia katika Quran hili kayaelezea mahusiano baina ya wana ndoa hawa wawili;
أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ ۗ
Mmehalalishiwa usiku wa Saumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao.
Mwenyezi Mungu amewasifia wana ndoa hawa mfano wa vazi, tutayataja sifa na kazi za vazi na kuelezea ni uhusiano upi uliopo baina ya mume na mke wake kusifiwa kama vazi ya kila mmoja kwa mwengine,
- vazi inasitiri; kama ambavyo nguo inasitiri kasoro na mapungufu nyingi tu yaliopo mwilini, vivo hivo mke au mume yuapaswa kuwa nguo kwa mwenzie, kusitiri aibu za mwenzako za ndani na za inje pia.
- vazi ni pambo; mara mwanadamu uvaa nguo ni kupendeza zaidi, na utamkuta atakapo amua kuvaa bora nguo, hatokuwa ni mwenye kupendeza na kuvutia, vivo hivo wanandoa wanapswa wafahamu kuwa, yeye kwa mwengine ni pambo, na iwapo atakua ni mwenye kumchafua mwengine kwa kutangaza mapungufu yake na siri zake mbele ya jamii, basi atakua ameharibu na amechafua pambo ile, na ndoa hio haitokua ni yenye kuvutia wala kupendeza baada ya hapo.
Mfano ulio bora kama funzo kwetu sisi ni yaliojiri katika kisa maarufu iliyojiri katika maisha ya Bwana wetu Mtukufu Mtume (saww), pambe ambapo wawili katika wake zake Mtume (saww) wanamfanyia hila kwa kutangaziana siri baina yao na kumuhadaa ili asiwe ni mwenye kula kitu fulani kwa nyumba ya mke wake Mtume kwa jina la Zainab alqibtiyyah, pale Mwenyezi Mungu aliposema;
وَإِذْ أَسَرَّ النَّبِيُّ إِلَىٰ بَعْضِ أَزْوَاجِهِ حَدِيثًا فَلَمَّا نَبَّأَتْ بِهِ وَأَظْهَرَهُ اللَّهُ عَلَيْهِ عَرَّفَ بَعْضَهُ وَأَعْرَضَ عَن بَعْضٍ ۖ فَلَمَّا نَبَّأَهَا بِهِ قَالَتْ مَنْ أَنبَأَكَ هَٰذَا ۖ قَالَ نَبَّأَنِيَ الْعَلِيمُ الْخَبِيرُ﴾
Na Nabii alipo mwambia mmoja wa wake zake jambo la siri. Basi alipo litangaza yule mke, na Mwenyezi Mungu akamdhihirishia Mtume, alimjuvya sehemu na akaacha sehemu nyengine. Alipo mwambia hayo, huyo mke akasema: Nani aliye kwambia haya? Mtume akasema: Kaniambia Mjuzi Mwenye khabari zote!
Iwapo hali ilkua hivi baina ya wake wa Mtume (saww), katika kuambiana siri baina yao, siri ambayo haikutoka inje ya ndoa, sasa itakua vipi katika kuitoa siri inje ya ndoa yako?
Ama kuna baadhi ya hali kwa kweli inakulazimu kusema siri ya jambo fulani ili kupata usaidizi, nasaha na utatuzi pale ambapo kwa kweli ni hali ya dharura, nayo inaruhusika tu kwa yule ambaye unayakini kuwa atawatatulia au atawasaidia kimaarifa na kimawazo kuhusu jambo fulani.











