Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.
1.MKE KUMUHUDUMIA MUME WAKE.
Katika mambo ya yalio na thawabu tele katika ndoa, ni Mke kumuhudumia mume wake,mke anapaswa ajitahidi jinsi atakavyo weza kumuhudumia mume wake, kwanzia kwa kumpokea anaporudi nyumbani toka kazini au shughuli yeyote ile, kumpokea kwa mapenzi na furaha adi mume ahisi kuwa kurudi kwake nyumbani ni furaha kwa familia yake, kumpa maji ya kunywa au ata chai kama atakua amesha andaa, kumpikia, kumuekea maji ya kuoga bafuni, na aina nyinginezo zozote ambazo yuaweza kumuhudumia mume wake ajitahidi kuyafanya, kwani kwa kufanya hivo, kunazidisha upendo ndani ya moyo ya mume wake kuona kuwa mke wake yuajitolea na kupambana kumshughulikia hali ya kuwa si wajibu wake.
Haipasi kwa wanandoa kuishi kwa kulipizana kwa maovu, mfano wa kwa kuwa nilikuambia uninunulie kitu fulani ila hukununua, hivo mimi pia sikupikii wala kukushughulikia, maisha ya mfano wa hayo kuyapelekea ndoa kutokosa amani na kila mmoja ufurahi kutokuwepo kwa mwenzake badala ya kinyume chake.
Mke yuapaswa kuangalia na kudhamini mambo yale yote mume wake anazojitahidi kuwapa na kushughulikia familia hio, kwanzia kwa makazi, mavazi, kuhakikisha watoto wanasoma vizuri na pia kuhakikisha nyumbani hakukosekani kitu, ni jihada ambalo lahitaji shukrani, na kama anavosema Mwenyezi Mungu (swt);
﴿هَلْ جَزَاءُ الْإِحْسَانِ إِلَّا الْإِحْسَانُ﴾
[ الرحمن: 60]
Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani?
basi mke pia ajitahidi na kuhakikisha kuwa anampa furaha mume wake pale anaporudi nyumbani, kwanzia kwa kumuheshimu na kumuskiza, wala hasiwe miongoni mwa wale wanawake ambao hawana shukurani na kumkemea pale anaporudi nyumbani ni riziki chache, kwani hadithi yatuambia;
– مَن لم يَشكُرِ القَليلَ؛ لم يَشكُرِ الكَثيرَ، ومَن لم يَشكُرِ النَّاسَ؛ لم يَشكُرِ اللهَ، التَّحدُّثُ بنِعمةِ اللهِ شُكرٌ، وتَركُها كُفرٌ، والجَماعةُ رَحمةٌ، والفُرقةُ عَذابٌ.
“Yule ambae hawezi akashukuru machache, hawezi akashukuru mengi, na yule hasieweza kumshukuru mja, hawezi akamshukuru Mwenyezi Mungu…”
Jambo lingine analopasa kulifanya mke ni kutomlinganisha mume wake na waume wengine, na kumdunisha kwa kumfanya kuwa wengine ndo wanaume pale wanapo timiza majukumu yao ilhali mume wake hajatimiza, hali hio haifai kabisa katika ndoa, si kwa mke pekee bali ata mume yuapaswa hasiwe katika hali hio, ni hali itayopeleka kila mmoja kujidharau na kujiona duni ndani ya nafsi yake.
Pale panapotokea sinto fahamu wa inapofikia wawili hao kukosana, wanapaswa watumie maneno mazuri katika kusuluhisha mambo yao na wala sio matusi na kukumbushana kila ovu alofanya mmoja katika maisha yao hio ya ndoa, Mwenyezi Mungu anatuambia katika Quran tukufu;
فَقُولَا لَهُ قَوْلًا لَّيِّنًا لَّعَلَّهُ يَتَذَكَّرُ أَوْ يَخْشَىٰ﴾
[ طه: 44]
Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa.
kwa kutumia maneno mazuri yaweza yakarudisha hasira ya mmoja wao au wote kutulia na kurudisha amani ndani ya nyumba hio.
Bwana Mtume (saww) anatuambia;
أيما امرأة رفعت من بيت زوجها شيئا من موضع إلى موضع تريد به صلاحا إلا نظر الله إليها، ومن نظر الله إليه لم يعذبه
Mwanamke yeyote, atakae nyanyua kitu, kutoka sehemu moja adi ingine, huku lengo lake kuu ni kumfurahisha mume wake, Basi M.Mungu hatokua ni mwenye kumuadhibu mwanamke huyo. Imam Baqir (as) anatuambia;
أيما امرأة خدمت زوجها سبعة أيام أغلق الله عنها سبعة أبواب النار وفتح لها ثمانية أبواب الجنة تدخل من أيها شاءت.
Mwanamke yeyote atakae muhudumia mume wake siku saba, Mwenyezi Mungu atamfungia milango saba ya motoni na atamfungulia milango nane ya peponi ili aingie kwa lango lolote atakalo taka.
Na zaidi ya riwaya hizi, kuna riwaya tele ambazo zaelezea ni utukufu na thawabu na ujira kiasi gani mwanamke anapata kwa kumuhudumia mume wake.











