Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu
3.HAKI YA NDOA
Miongoni mwa haki za kushirikiana baina ya pande zote mbili, ni haki ya ndoa. Kama ambavyo tulitaja na kuelezea kuwa ni lazima kwa mume kumpa mke haki ya ndoa, vivyo hivyo ni lazima zaidi na juu kwa mke kumpa mume haki hio, hadithi tuliotaja kutoka kwa Bwana Mtume (saww) akielezea haki za mke kwa mume wake, amesema kuwa;
جاءت امرأة إلى النبيّ صلى الله عليه وآله وسلم فقالت: يا رسول الله! ما حق الزوج على المرأة؟ فقال لها: أن تطيعه، ولا تعصيه، ولا تتصدق من بيته، إلا بإذنه، ولا تصوم طوعاً إلا بإذنه، ولا تمنعه نفسها وإن كانت على ظهر قتب، ولا تخرج من بيتها الا بإذنه، وإن خرجت بغير إذنه لعنتها ملائكة السماء وملائكة الأرض، وملائكة الغضب، وملائكة الرحمة حتى ترجع إلى بيتها، قالت: يا رسول الله! من أعظم الناس حقاًّ على الرجل؟ قال: والده قالت: فمن أعظم الناس حقاًّ على المرأة؟ قال: زوجها، قالت: فما لي عليه من الحقِّ مثل ما له عليَّ؟ قال: لا، ولا من كل مئةٍ واحدة”
Katika hadithi Bwana Mtume (saww) anaonyesha ni kwa kiwango gani mke anapaswa kumpa mume wake haki hio ya ndoa, pale alipotaja;
ولا تمنعه نفسها وإن كانت على ظهر قتب،
Na wala (mke) hasimzuie mume wake nafsi yake (hasimnyime tendo la ndoa) ata kama ni juu ya ngamia (kwa hali yeyote ile).
Mwanamke anapaswa ampe mume wake haki hio ya ndoa mahala popote panapokubalika kisheria, iwapo mume wake atakuwa ni mwenye kuitajia, na kwa nyakati zote, ila wakati ambapo mke huyo yupo katika hali yake ya hedhi.
Mwanamke anapaswa wanapokuwa kitandani au anapokuwa kitandani, ajiweke kwa hali ya kumvutia mume wake kwa kitendo hicho na kumfanya mume wake awe na hamu nayo, na wala hapaswi kujiweka kwa hali ya kinyume cha hicho, au kumfanya mume wake awe ni mwenye kunyeyekea na kumuomba ili ampe haki hio.
Ni makruhu na linakera zaidi kwa mwanaume kumlazimisha mke wake katika tendo la ndoa ilhali mke wake hataki au hana hamu nayo, katika hali hio, ata lile malengo la tendo la ndoa halitakuwa ni lenye kupatikana wala ule asali wa tendo hilo halitokuwepo wala halitapatikana. Ila hisifahamike vibaya kwa wanawake na wakatumia nafasi hio kuwanyime waume zao tendo hilo kwa jina kuwa wanalipiza kisasi kwa mfano au wamekerena ama mume amekosa kumpa au kumnunulia mke wake kitu, ikawa ni sababu ya mke kumnunia na kutumpa haki hio kwa jina kuwa hana hamu na kitendo hicho. Bali wawili hao, wanandoa hao wanapeswa waishi kwa mapenzi na huruma daima, iwapo kutakua na mapenzi baina yao jambo hilo la mke kumzuia mume wake haki hio halitokuwa ni lenye kutokea.
















