Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
Katika nakala zilizotangulia,tulizungumzia na kuyaelezea kwa mapana haki za mume kwa mke wake, ama kwa nakala huu, na nakala zifuatazo, tutayataja na kuyajadili haki za mke kwa mume wake, kwa maana mambo yapi ambayo yanayompasa mke kumfanyia mume wake.
Miongoni mwa haki hizo ni;
1.KUMTII NA KUTOMKAIDI
Mwanamke au mke, anatakiwa awe mtiifu kwa mume wake, utiifu kwa maana mume wake atakapomuamrisha jambo atakuwa ni mwenye kuskia na kuyafanya, vile vile, mke hatakiwa kukaidi amri ya mume wake, hasa mume anapoyaitaji au kumuamrisha mambo yanayohusu haki zake mume, mfano wa haki la tendo la ndoa, Mke hapaswi kumkaidi na kumnyima mume wake tendo la ndoa pale ambapo mume wake atakuwa ni mwenye kuitajia tendo hilo, vivo hivo kwa haki zinginezo.
Ama jambo linalopaswa lifahamike kwa makini sana ni kuwa, tunapozungumzia kuwa mke anapaswa awe mtiifu kwa mume wake, utiifu huu, haujumuishi mambo yanayoenda kinyume na sheria ya kiislamu, mfano haiwezekani kwa mume kumuamrisha mke wake kuwa hasisali, au hasifunge saumu zake za wajibu, au mume anapomtaka mke ilhali mwanamke huyo yuko katika hali ya hedhi, mwanamke haruhusiwi kumtii mume wake kwa mambo haya na kwa mfano wa hayo, kwani Imam Ali (as) anatuambia kuwa;
لَا طَاعَةَ لِمَخْلُوقٍ فِي مَعْصِيَةِ الْخَالِقِ
Hakuna utiifu kwa kiumbe (anapokuamrisha) kumuasi Muumba.
Ama iwapo itatokea kuwa mwanamke amekosa kumtii mume wake, katika yale mambo ya haki zake, na ambayo hayaendi kinyume na sheria zake Manani, Mume hapaswi kumpiga kama ambavyo imezoeleka katika jamii yetu ya sasa, bali yuapaswa mume huyo, afate yale hatua yalotajwa ndani ya Quran tukufu, na ambazo pia tulizitaja katika nakala zetu ziizo tangulia, mwanzo anapaswa ashauriane nae na kumuelezea, kisha baada ya hapo afate hatua zilizotajwa.
Ama katika kuelezea na kusisitizia jambo hili, tutataja hadithi kutoka kwa Mtume (saww) amesema;
جاءت امرأة إلى النبيّ صلى الله عليه وآله وسلم فقالت: يا رسول الله! ما حق الزوج على المرأة؟ فقال لها: أن تطيعه، ولا تعصيه، ولا تتصدق من بيته، إلا بإذنه، ولا تصوم طوعاً إلا بإذنه، ولا تمنعه نفسها وإن كانت على ظهر قتب،
Mwanamke alimjia Bwana Mtume (saww), kisha akamuuliza Mtume, Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! ni yapi haki za mke kwa mume wake, Mtume akamwambia, Mke huyo awe Mtiifu, na wala hasimuasi mume wake, na wala hasitoe sadaqa katika nyumba yake mume, ila kwa idhini yake, Na wala hasifunge (funga za mustahabu) ila kwa idhini yake, na wala hasimnyime nafsi yake (mke hasimnyime mume wake tendo la ndoa) ata kama watakua katika juu ya ngamia (ata kama watakua katika haki ngumu mfano wa juu ya ngamia)
















