Follow us in
Follow us in

HAKI ZA MKE KWA MUME WAKE (2)

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.

Katika nakala iliotangulia, tulianza na tukajadili miongozi mwa haki zinazompasa mke kumfanyia mume wake, tulitaja haki ya kwanza ambayo ilikuwa ni lazima kwa mke kuwa mtiifu kwa mume wake na wala hasiwe ni mwenye kukaidi amri yake mume wake, ama katika nakala hii, tutaendeleza haki hizo na kuzifafanua kwa upana ili ifahamike kwa urahisi, miongoni mwa haki hizo ni;

2.KUAMILIANA NA MUME WAKE KWA WEMA

Kama ambavyo tulitaja na tukaelezea haki hii, pale tulipotaja haki za mume kwa mke wake, haki hii ni yenye kushirikiana, vivo hivo yampasa mke awe ni mwenye kuamiliana na mume wake kwa wema, Mke yuapaswa ahakikishe kuwa uhusiano wake na mume wake uwe ni uhusiano wa kupendeza na kufurahisha daima, mume anapoingia au kurudi nyumbani anapata mazingira ni yenye kupendeza, kwa kufanya hivyo, mume huyo atafurahia daima kubaki nyumbani kwani mazingira yale tayari yanampa furaha na amani.

Imam Ali (as) anatuambia;

الإمامُ عليٌّ عليه السلام :جِهادُ المَرأةِ حُسْنُ التَّبَعُّلِ

Jihadi ya mwanamke ni kuhakikisha kuwa anaishi na mume wake vyema

Mke anapaswa amfanyie mume wake mambo ambayo yanampendeza mume wake na wala sio kumtusi, kumdharau au kumsema vibaya mume wake kama ambavyo kwa bahati mbaya ndo imekua mazoea ndani ya jamii yetu, ambapo utampata ata mke wa mtu anafikia hatua ata ya kumpiga mume wake au ata kumchoma kwa maji moto na zaidi ya hayo. Mke anatambulika kama mlinzi wa nyumba, hivyo anaweza kusababisha nyumba yake ikawa moja katika nyumba za peponi na vivo hivo aweza kufanya pia nyumba yake ikawa moja katika nyumba za motoni.

Katika madhumuni ya riwaya imepokelewa kuwa, kuna mambo matatu ambazo ambazo mke akimfanyia mume wake anapata ujira matatu,

Jambo la kwanza, mke anatakiwa awe ni mwenye kumpokea mume wake pale anaporejea kutoka kazini au miongoni mwa shughuli zake, wala hapaswi mke kumtuma mtoto au mume mwenyewe kujifunguliwa mlango pale anaporudi. Pili mume akitoka awe ni mwenye kumsindikiza na kuhakikisha kuwa mume wake anatoka kwa hali ya kupendeza na kwa manguo iliopendeza na Tatu au la mwisho mke anatakiwa awe ni mwenye kumliwaza mume wake, pale anapomuona mume wake ni mwingi wa mawazo awe ni mwenye kumuondolea mawazo hayo, kwa kufanya hivyo, Mwenyezi Mungu (swt) amembashiria pepo mwanamke kama huyu, pili ni kuwa, M.Mungu (swt) umfanya kuwa miongoni mwa watumishi wake yeye (swt) na tatu na la mwisho, kila siku uandikiwa thawabu ya mashahidi sabini.

Hivyo basi tunaona ni kwa namna gani Mwenyezi Mungu (swt) amesisitizia mke kuashi na mume wake kwa wema, na ni thawabu teletele namna gani kwa kufanya jambo hilo mwanamke anakuwa ni mwenye kuyapata.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Best Topics

Hotest Now

اشترک فی الاجتماعایت

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

للتحمیل اضغط هنا

الرابط المباشر

شارک مع الآخرین :