Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.
4. HAKI YA MUME KUMUHESHIMU MKE
Miongoni mwa haki za mke kwa mume wake, ni mume awe ni mwenye kumuheshimu mke wake, kinyume na mambo na fikra za hali ya sasa, ambapo wanaume ufikiri kuwa wao pekee ndo wanapaswa kuheshimiwa, jambo ambalo kutokana na Quran tukufu tunaona ni kinyume ilowazi, Mwenyezi Mungu atuambia katika Quran;
هُنَّ لِبَاسࣱ لَّكُمۡ وَأَنتُمۡ لِبَاسࣱ لَّهُنَّۗ
Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao.
sura baqara;187
Mwenyezi anatuambia kuwa wake zetu ni vazi yetu, na kama ambavyo inafahamika kuwa kazi ya vazi ni kusitiri, hivyo kama ambavyo sisi ni sitara kwao, wao pia ni sitara kwetu, na tunapaswa kusitiriana mapungufu na udhaifu wowote unaopatikana kutoka pande zote mbili.
Bwana Mtume (saww) anatuambia;
حَقُّ المرأةِ على زَوجِها أن يَسُدَّ جَوعَتَها ، و أن يَستُرَ عَورَتَها ، و لا يُقَبِّحَ لَها وَجها
Haki ya mke kwa mume wake ni kuwa hamuondoe katika hali ya njaa, (ampee chakula) na asitiri siri zake (ampe haki ya tendo la ndoa) na wala hasimkunjia uso (hasionyeshe hali ya kukereka(amueshimu))
Na Yeye yeye bwana Mtume saww amesema;
من تزوج امرأة فليكرمها
yeyote atakae oa mwanamke, basi ahakikishe amemkirimu.
Ama katika mambo ambayo yanapaswa yafahamika pale wanapokusudia kuwa unamheshimu mwanamke, ni kuwa husiongee mambo ya mke wake inje, kupeleka mapungufu ya mke wako kwa marafiki zako au ata kwa watu wako wa karibu, jambo hili ni jambo la kusikitisha kwa kweli, na ni jambo la kumdhalilishe mkeo, wapaswa ufahamu kuwa, mkeo anapodhalilika ndo wewe pia umedhalilika, mwapaswa kusitiriana kwani ninyi ni vazi la mwengine.
5.HAKI YA MUME KUJIWEKA KATIKA MAZINGIRA MAZURI KWA AJILI YA MKE WAKE
Kinyume na mawazo ya wengi, kuwa suala la kujipamba na kujiweka katika mazingira mazuri, ni suala linalo wahusu wanawake pekee, jambo hili ni jambo ambalo ni la lazima na la msingi kwa mume pia kujiweka katika mazingira nzuri kwa ajili ya mke wake,
Mwanaume anapaswa ajipambe kwa ajili ya mke wake, iwe ni kuchonga ndevu, chanua nyele zake,kuvaa nguo nzuri mbele ya mke wake, kunyoa, kuoga na kufanya mengine mengi ambayo yatamueka katika mazingira ya kupendeza pale atakapokuwa amesimama mbele ya mke wake, wala sio mwanaume kunuka jasho, kuvaa manguo mazuri anapotoka kuelekea kazini pekee na anapokuwa na mkewe anavaa manguo yaliochakaa,hachani nyele wala kuwa msafi anapokuwa na mkewe, mwanaume anapaswa awe na nguo ya nyumbani, nguo ambayo mke wake anapenda pale anapomuona amevalia nguo hio. katika riwaya, imam Ali (as);
حسن بن جهم:رایت اباالحسن (ع) اختضب، فقلت: جعلت فداک! اختضبت؟ !فقال: نعم، ان التهیة مما یزید فی عفة النساء، و لقد ترک النساءالعفة بترک ازواجهن التهیة. ثم قال: ایسرک ان تراها علی ماتراک علیه اذا کنت علی غیر تهیة؟قلت: لا. قال: فهو ذاک. ثم قال: من اخلاق الانبیاء، التنظف و التطیب وحلق الشعر و کثره الطروقة؛
Katika kujipamba na kuvaa vizuri kwa mwanaume, ni katika mambo yanayo mpelekea mwanamke kijihifadhi
Mwanamke awe anapokuona anafurahia, anapokuwa karibu nawe anaskia harufu nzuri ya marashi au mafuta yanayonukia, mwanamke anapokuwa katika hali hii, anatosheka nawe na hatokuwa na haja ya kuangalia pengine au kutafuta mazuri mahala pengine. Na unapojiweka katika hali hii, inamfurahisha sana mke kama ambavyo mwanaume unavofurahi pale unapompata mke wake amejiweka katika mazingira mazuri kwa ajili yako, amejipamba na kujirembesha kwa ajili yako pekee.
















