Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
MAMBO YA ADABU AMBAYO MUME ANAPASWA KUMFANYIA MKE WAKE.
- Mume kumlisha mke wake chakula kwa mkono wake
Katika mambo yanayo zidisha mapenzi katika ndoa, na kufanya wanandoa hao kuwa karibu zaidi kihisia, ni kula pamoja daima, wanandoa wanapaswa wale kwa pamoja, na pale wanapokula wawe ni wenye kulishana baina yao, kitendo hiki ni kinyume na mawazo ya wengi ambao wanaamini kuwa yamepitwa na muda na ni kupoteza muda, bila kufahamu kuwa kwa kufanya hivyo kando na kuongeza mapenzi, wanandoa hao wanapata thawabu teletele kutoka kwa Manani.
Bwana Mtume (saww) anatuambia;
إنَّ الرَّجُلَ لَيُؤجَرُ في رَفعِ اللُّقمَةِ إلى فِي امرَأتِهِ
“Hakika mwanaume yuapata thawabu, kwa kunyanyua mkono wake na kumlisha mke wake.”
hivyo basi ni juu ya mwanaume kujitahidi walau ata kama si kila siku, walau mara moja kwa wiki, awe ni mwenye kumlisha mke wake kwa kupitia mkono wake chakula.
- kuwa na wakati wa kuketi na mkeo
Mume anapaswa atafte muda daima kwa ajili ya kuketi na mke wake tu, ili kubadilishana mawazo, kuchekeshana n.k, jambo hili ni muhimu sana kwa maisha ya wanandoa, ama katika ulimwengu wa sasa, khususan pale ambapo wanandoa wote wawili wamejishughulisha na kazi, wanakosa fursa wa kuketi kwa pamoja jinsi inavyofaa, kwani wakati wanapopata ni usiku pekee, kila mmoja amechoka na utaka kupumzika, asubuhi na mapema kila mmoja ameelekea kazini, katika hali hii, inawalazimu na ni jambo la dharura kwa kweli watafute ata kama ni siku za mapumziko waketi kwa ajili ya kuzungumza maisha yao, kufurahishana na kubadilishana mawazo.Na kwa kupitia njia hii ndipo utakapo fahamu yale magumu anayoyapitia mwenzako ima iwe ni kazini,nyumbani au ata maishani.
Bwana Mtume (saww) anatuambia;
جُلُوسُ المَرءِ عِندَ عِيالِهِ أحَبُّ إلَى اللّه ِ مِنِ اعْتِكافٍ في مَسجِدي هذا
Mtu kuketi na familia yake, ni bora zaidi kwa Mwenyezi Mungu kushinda mtu kuketi itikafu ndani huu msikiti(msikiti wa bwana Mtume saww)
kupitia hadithi hii, tunafahamu kuwa, zaidi wanandoa kubadilishana mawazo, kutulizana na kufurahishana, kuna thawabu chungu nzima pale mmoja anapoketi na mkewe, bali si hivyo tuh, ni jambo ambalo linapendwa na Mwenyezi Mungu (swt)
Hadithi hii inaashiria ni kwa namna gani Uislamu umetilia mkazo suala la mtu kuketi na mkewe.
- Kumsaidia mkeo katika shughuli za nyumbani
Mume wapaswa ufahamu kuwe shughuli za nyumbani si wajibu wa mke wake kutimiza, yani miongoni mwa haki zako kwake, hio haipo, hivyo basi wapaswa kumsaidia mkeo katika shughuli za nyumbani bali si kuketi na hali mkeo uataabika kufanya shughuli zote.
Ndoa yapaswa iwe ya mapenzi, na daima mpenzi hapendi kumuona mwenzie akitaabika katu, bali wapenzi ni pale wanapo saidiana kimawazo, kimatendo na katika kila shughuli iliowazunguka wawili hao.
Mfano mzuri wa kuigwa, ni kisa ya mtume saww pale alipoenda kwa nyumba ya binti yake fatima as, akampata Imam Ali(as) (Mume wake Fatima as) akiwa anamsaidia mke wake, jambo hilo mtume alilisifia na kuashiria thawabu tele inayopatikana pale mume anapomsaidia mke wake katika shughuli za nyumbani.
















