Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi Wa Rehema Mwenye Kurehemu.
Katika kuyaendeleza msururu wa nakala zetu, zinazohusu haki za wana ndoa baina yao wawili, kulizungumzia haki za mke kwa mume wake yani mambo yanayompasa mke kumfanyia mume wake, leo tutazungumzia haki muhimu na ambayo imechukuliwa kwa kinyume yake katika jamii yetu ya hivi sasa, nayo ni;
MWANAMKE KUJIANDAA NA KUJIREMBESHA KWA AJILI YA MUME WAKE;
Kinyume na inavofanyika leo hii na haswa katika jamii yetu ya afrika mashariki, mwanamke ujipamba na kijirembesha na kila aina ya mapambo pale anapotaka kutoka inje ya nyumba yake na kuwatembea jamaa au kuhudhuria harusini na sherehe nyinginezo, sababu ya kufanya hayo yote ni kila mmoja amuone na atambue uzuri alokuwa nayo amsifie, kando na kufahamu kwa kufanya hivo yupo chini ya laana yake Mwenyezi Mungu (swt) pale mtume Muhammad (saww) anapotuambia;
قال رسول الله (صلى الله عليه وآله): أي امرأة تطيبت وخرجت من بيتها فهي تلعن حتى ترجع إلى بيتها متى ما رجعت.
Mwanamke yeyote, atakae jirembesha na kujipamba, kisha akatoka inje ya nyumba yake, basi afahamu kuwa yuko chini ya laana adi pale atakapo rejea nyumbani mwake.
Ama jambo ili kwa kweli limesahaulika na kupuuziliwa na dada zetu pamoja ata na kina mama zetu ndani ya jamii yetu ya afrika mashariki bali ulimwenguni kwa ujumla. Jamii zetu za sasa hivi ata wanapotoka nyumbani si kujirembesha wala kujipamba tu, bali ata yale mipaka na migezo wanavopaswa kuyasitiri ata uwa hawayasitiri, utawapata wanatoka nyumbani na masuruali huku kichwani kupo wazi, jambo ambalo Mwenyezi Mungu amelikemea na kuliharamisha, pale anaposema Mwenyezi Mungu ndani ya kitabu yake Tukufu;
﴿وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُولِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَىٰ عَوْرَاتِ النِّسَاءِ ۖ وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ ۚ وَتُوبُوا إِلَى اللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa.
Katika kuyafafanua aya,” wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika.” sehemu unao dhihirika ni viganja vya mkono na mguu pamoja uso, zaidi ya hapo inampasa mwanamke anapotoka awe ni mwenye kujusitiri kwa sitara inayofaa na inayokubalika kisheria.
“wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke.” Sheria ya Mwenyezi Mungu ambayo ipo wazi, mwanamke yuapaswa kujipamba na kujirembesha mbele ya mumewe na wale ambao ni maharim wake pekee, zaidi ya hapo anakua ni mwenye kupata dhambi kwa kuyafanya hayo.
Zaidi ya hayo, hadithi zipo tele zinazoelezea ubora na thawabu anazopata mwanamke ambae katumia muda wake kwa kijirembesha kwa ajili ya mume wake, kwani kwa kufanya hivo anazidisha mapenzi ndani ya moyo ya mume wake na anajaalia ndoa yake inakua ni yenye furaha na bashasha.











