Follow us in
Follow us in

UMUHIMU NA MALENGO WA KUOA KATIKA DINI YA UISLAMU

Kwa Jina La Mwenyezi Mungu Mwingi Wa Rehma Mwenye Kurehemu

Mwenyezi Mungu {swt} katika Quran tukufu amesema:

وَمِنْ ءَايَٰتِهِۦٓ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَٰجًا لِّتَسْكُنُوٓا۟ إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةًۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَءَايَٰتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

“Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.”

surat rum:21

Pale ambapo mmoja anakua ni mwenye kumtafuta na kuutafuta njia za kumfikia Allah{swt},kudhibitisha uwepo wake inatumika dalili aina tofauti tofauti,moja ya dalili ambazo amezitaza Allah[swt}katika kitabu chake kitukufu ni kuwe Yeye{swt} amekuwa ni mwenye kutuumbia sisi,kutokana na nafsi zetu, wake,na akawa ni mwenye kujaalia kupatikana mapenzi na huruma baina wa mume na mke pale wanapokuwa wameoana.

Hivo basi tunaona kuwa kuna vitu vitatu vikuu ambavyo ni muhimu na ndo msingi wa ndoa ulosawa, ndoa itakayo dumu daima kuwa navyo,navyo na vile alivyovitaja Yeye{swt}:

  • Utulivu
  • Mapenzi
  • Huruma

Hivo basi,tutazungumzia na kuelezea walau kwa mukhtasari,yale aliyokusudia Allah{swt} kutokana na utulivu,mapenzi na huruma katika ndoa,na ni vipi tunaweza kuimarisha na kuiweka ndoa yetu iwe na misingi yote hayo matatu.

  1. UTULIVU

Katika maumbile ya mwanadamu,ni kwamba ameumbwa akiwa na mapungufu aina fulani,mapungufu hayo yanaondoka pale tu mwanadamu atakapo patana na mwenzake,awe ni mwanaume au mwanamke,mwanaume hawezi kuwa au sio mkamilifu ila adi pale atakapopatana na mwenzie.

Kwa njia ingine,mwanamke yuko na uwezo wa kupata mtoto,alivyomuumba Allah {swt} vivo hivvo mwanaume yuko na uwezo wa kupeana ujauzito,hivyo basi kila mmoja anamtegemea mwenzie katika kumwezesha afikie malengo yake,na kwa wao kuwa pamoja,wanakuwa wamehitimisha yale yanayoitajika kwa kupatikana kwa mtoto.Kwa sababu ya kutokamilika huku,ndiko umsababisha kila mmoja kumtafta mwenzie na adi pale atakapo mpata ndipo anapopata amani na utulivu.

Ata hivo kile ambacho hakijakamilika,daima kinatafta njia ili kiweze kufikia ukamilifu,na yule ambaye yuko na haja,daima utafta njia ili aweze kufikia na kukidhi haja na mahitaji zake.

2.MAPENZI

Imam Ja’afer Sadiq a.s. amesema:
“Mimi nina uhakika kuwa mtu anapokuwa bora zaidi katika imani na Islam basi vivyo hivyo mapenzi ya wake zake inavyozidi.

Aya isemayo: Allah swt ameweka mapenzi na huruma baina yenu, inaonyesha kuwa mapenzi ya kindoa ni baraka za Allah swt; na vile mtu atakavyokuwa na imani zaidi katika Allah swt, ndivyo vivyo rehema na baraka zaidi za Allah swt zitakuwa juu ya jozi hiyo (yaani bibi na bwana ).

Na kwa sababu hii Imam Ja’afer Sadiq a.s. amesema:”Miongoni mwa desturi za Mitume ni mapenzi ya wanawake.”

Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema, “Ijulikane mtu bora miongoni mwenu ni yule ambaye ni bora kwa wake zake na mimi ni bora kwa wake zangu.”

Vivyo hivyo ameendelea kusema: “Rehema na baraka za Allah swt ziwe juu ya mtumwa wake ambaye anawafanyia wema baina yake na mke wake kwa hakika, Allah swt amempa mamlaka zaidi juu ya mke wake na kwamba amemfanya awe ni mtu mwenye kumhifadhi mke wake.”

Kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, imesisitizwa kuwa mwanamme anapokuja nyumbani aje na uso wenye bashasha, mchangamfu. Nyumba hiyo itakuwa ni Jannah iwapo sheria kama hizi zitafuatwa kwa makini.

3.HURUMA

Ndoa inajumuisha watu wawili,mwanaume na mwanamke,watu wawili ambao wamelelewa katika mazingira na malezi tofauti tofauti kabisa na ya mwengine,mara nyingi ata wale wale ambao wamelelewa katika familia moja na malezi moja bado kuna mvurugano,vita na kutoelewana kwingi,itakua vipi kwa watu wawili ambao wamelelewa kutoka kwa familia na mazingira tofauti?

hivo basi inawapasa wanandoa awa wawili,wawe na huruma baina wao kwa wao,Na ili huruma hii iweze kupatikana ni lazima kila mmoja wao aweze kutambua nafasi yake kwa mwenzie,mume atakapojua ni nafasi ipi,wajibu upi alonao kwa mke wake,na mke vivo hivo,huruma inaweza kupatika na kujengeka baina ya wanandoa.

Mume anatakiwa amhurumie mke wake kipindi amechoka na yale mapungufu yake ya kibinadamu,na kumsamehea na kumrekebisha kwa makosa yake,na vivo hivo,mke anatakiwa kufanya hivo,na kumhurumia mume wake kipindi ana msongo wa mawazo na yale mapungufu yake ya kibinadamu.

 

FAIDA YA NDOA

Bwana mtume{saww} amesema:

“ما استفاد امرء مسلم فائدة بعد الاسلام أفضل من زوجة مسلمة تسره إذا نظر إليها وتطيعه إذا أمرها وتحفظه إذا غاب عنها في نفسها وماله”

Anatuambia mbora wa viumbe,mwana wa Abdullah{saww}kuwa,hakuna kitu anachofaidika nacho zaidi mwislamu,baada ya uislamu,anapopata mke mbora,anapokuwa akimtazama mwanamke huyo,umfurahisha na kumpea furaha,na pale anapomuamrisha anakuwa ni mwenye kumti na kutii amri zake,na anakuwa ni mwenye kujihifadhi,pale ambapo anapokuwa mbali nae,anakuwa mwaminifu na wala hamsaliti,analinda nafsi yake na pia kulinda mali ya mume wake.

Kutoka kwa haya tuona kuwa kuwa na mke jambo muhimu sana na lenye faida na kuleta furaha katika maisha ya mwanadamu,katika riwaya imeripotiwa kuwa Imam ali{as} amesema;

‘و لقد کنت انظر الیها فتکشف عنی الهموم و الاحزان”

Kuwa pale Imam ali as alikuwa na huzuni na uchovu,alipokuwa akirudi nyumbani kwa kumtazama Bibi Fatima{as} uchovu pamoja na uzuni ulikuwa unaondoka na anakuwa ni mwenye kupata raha na furaha kwa kumtazama Bibi Fatima{as}

Katika ahadith tunaambiwa kuwa mwanamke anaweza akageuza nyumba yake kuwa moja kati ya bustani za pepo,na pia anaweza akabidi nyumba yake ukawa ni moto mkali wa jahanamu,hivo ni wajibu wa mwanamke kuandaa nyumba yake na kuandaa mazingira kwa mume wake pale atakapokuja apate mazingira ni mazingira ya furaha.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Best Topics

Hotest Now

اشترک فی الاجتماعایت

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

للتحمیل اضغط هنا

الرابط المباشر

شارک مع الآخرین :