Follow us in
Follow us in

MALEZI KWA WATOTO

MALEZI YA WATOTO

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

Katika msururu wa nakala zetu zilizotangulia, tulizungumzia kwa uwazi na upana zaidi maisha ya ndoa, faida za kuoa au kuolewa na haki zinazowahusu wana ndoa hao, ama katika nakala hii, na nakala zitakazo fata tutazungumzia jambo muhimu sana ambayo si msingi pekee inayomuunda mwanadamu, bali ndo msingi inayoiunda jamii kwa ujumla, ili kupata jamii yenye amani, utulivu na upendo baina ya wanainchi na raia wa jamii hio, ni lazima katika malezi ya raia ya wanajamii hao, wawe wamepata malezi inayofaa, ambayo malezi hio ndo ima iwe sababu ya jamii hio kufaulu au kudidimia.

Kama ambavyo Mwenyezi Mungu (swt) anatuambia;

وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا

Mwenye kuuhisha nafsi, ni kama vile(ni sawa na) amehuisha watu wote ulimwenguni.

Katika malezi ya watoto, kwanzia kuzaliwa adi pindi atakapo kuwa mtu mzima, imegawanyika katika hatua tatu tofauti;

1.Hatua ya kwanza: Nayo ni pindi mtoto anapozaliwa adi atakapo fikisha miaka saba, ambapo kwa hatua hii, mtoto upewa jina “mfalme(raisi, mkubwa au kiongozi)”

2.Hatua ya pili: Nayo ni kwanzia miaka saba adi miaka kumi na nne ya mtoto huyo, katika kipindi hiki, mtoto upewa jina “mtumwa”

3.Hatua ya tatu: Kwanzia miaka kumi na nne adi miaka ishirini na moja ya mtoto huyo, ambapo katika hatua hii au kipindi hiki, mtoto upewa jina “waziri”

HATUA YA KWANZA KATIKA MALEZI

Katika hatua hii, kama ambavyo tumeashiria hapo juu, ni hatua inayoanza pindi mtoto anapozaliwa adi atakapofikisha miaka saba, malezi katika hatua hii, ni muhimu sana na ndo nguzo au mzizi wa maisha wa mtoto huyo, iwapo katika hatua hii mtoto akapata malezi mbovu na isiofaa, itamjaalia mtoto huyo mbeleni katika maisha yake kuwa na maisha yenye matatizo na upungufu. Hivo basi, kama tulivoashiria, katika hatua hii mtoto uwa ni mfalme,raisi, au kiongozi, na anapaswa kuchukuliwa kama mfalme na wazazi wake, yani kile atakachokuwa yuataka anapewa, na kama ambavyo mfalme uwa yuko na waziri wa kumshauri katika kila suala, na kumuelezea madhara na faida ya jambo fulani na fulani, au kufanya na kutofanya kwa jambo hilo, vivo hivo wazazi wanapaswa kuwa ni waziri wa mtoto huyo katika hatua hii, wawe ni kumuelekeza husifanye hii, madhara ya kufanya jambo hili ni lipi na ni lini wakati muafaka wa kufanya jambo hilo na mfano wa hayo.

Bali katika jambo la kuzingatia, hupaswi kumuambia mtoto katika hatua hii, moja kwa moja kuwa husifanye jambo fulani, fanya hii, husifanye hii, kama ambavyo ilivozoeleka katika jamii yetu, katika kumuamrisha mtoto hio ni hatua ingine itakayofuata, ama katika hatua hii, mtoto ni mfalme, kama ambavyo huwezi kumuambia mfalme husifanye hili, fanya hili, vivo hivo ndo utamuambia mtoto, kwa njia ya hekima.

Katika kuzingatia na kumlea ipasvyo mtoto katika miaka saba ya kwanza, utapata utulivu katika hatua ya pili na hatua ya tatu katika malenzi, kama ambavyo tuliashiria kuwa hatua hii ndio msingi wa maisha wa mtoto huyo.

Katika madhara ya kumlea mtoto kimakosa katika hatua hii, ni kuwa, mtoto atakosa kujiamini katika maisha yake, na atabali katika hali ya kuamrishwa tu, bali hawezi kuwa na uhuru wa kujiamulia cha kufanya katika jambo mingi katika maisha yake.

Miongoni mwa jambo la kuzingatiwa tunaposema kuwa mtoto ni mfalme katika hatua hii ni kuwa, kama ambavyo mfalme yuko daima na watu wa kumsaidia na kumpa vitu kila mara anapohitajia katika harakati zake, vivo hivo ndivo alivo mtoto, mzazi yuapaswa kuwa naye daima na kumuhudumia kwa kumpa chochote atakachoitajia, sawa iwe ni chakula au ni katika vitu vya kuchezea vya mtoto huyo.

Katika mfano ingine katika malezi, ni kumpa mtoto katika hatua hii muda unaofaa na kumtengezea mazingira iliotulia, ambayo haina kelele wala usumbufu ili mtoto awe ni mwenye kupumzika, kwa kufanya hivo, utampa mtoto huyo utulivu wa nafsi na akili, ambazo ni misingi yanayohitajika katika kumlea mtoto huyo.

Mtoto katika hatua hii, anaitajia mapenzi zaidi, kuonyeshwa mapenzi kutoka kwa wazazi wake, huu ndo msingi wa maisha wa mtoto huyo, iwapo katika msingi wake, atakosa mapenzi ya mzazi au wazazi wake, athari hio itamuathiri katika maisha yake na kuathiri mahusiano, maelewano na ukaribu baina yake na wazazi wake.

Katika jambo lingine la kuzingatia na la muhimu sana, ni kuhusu kuwapiga watoto katika hatua hii, kinyume na ilivozoeleka na jamii, ambapo mtoto upigwa na kuchapwa kuanzia udogoni ata uzeeni madamu anasifa ya kuwa bado yuko mtoto, jambo ili ni kosa kabisa katika malezi, mtoto wa hatua hii tulotaja hapaswi kupigwa kamwe, sababu na hoja ni kuwa, katika hatua hii mtoto ujifunza kutokana na mazingira aliopo, kutokana na yale yote yanayofanyika nyumbani anayoyatazama, kuyaskia nakadhalika, hivo basi, kwa kuwa na ada ya kumpiga mtoto uzidisha mazoea katika maisha ya mtoto huyo na kufanya kuwa kupigwa kwa ni jambo la kawaida ata katika hatua zingine zitakazofuata katika maisha yake, na hatokuwa ni mwenye kuichukulia kama onyo au amrisho ya kusisitiza.

Kama ambavyo tumeguzia kuwa, watoto katika hatua hii wanajifunza kutokana na vitu wanavyo vitazama nyumbani, au vitu wanavyosikia, hivo basi, mambo watakayo fanya wazazi wake katika hatua hi, watoto wale watakua wakijifunza kwayo, iwapo wazazi watakua ni wenye kusali, watoto pia watakua ni wenye kusali, na iwapo wazazi watakua ni wenye kugombana daima, kutukanana na ata kupigana mbele ya watoto, jambo hilo daima litabaki na litamuathiri mtoto huyo ata katika maisha yake ya baadae au ata pale atakapo kuwa katika ndoa yake.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Best Topics

Hotest Now

اشترک فی الاجتماعایت

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

للتحمیل اضغط هنا

الرابط المباشر

شارک مع الآخرین :