Follow us in
Follow us in

ADABU ZA MKE KWA MUME WAKE (2)

2.KUWA NA SUBRA KWA MAUDHI YA MUMEWE

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.

Katika mke kumvumilia na kuwa subira katika yale anayoyafanya mume wake, kuna thawabu na ujira teletele ambazo anazipata mwanamke huyu kwa kuyafanya hayo. Kama tunavyojua kuna baadhi ya wanaume ambao wanafurahi kuwaudhi wake zao kila mara kwa maudhi tofauti tofauti, ima ni awe mkorofi, jabali, yuko na tabia mbovu au ata daima hacheki wala ata kutabasaamu, haya ni mambo ambayo kwa kweli yanaitajia subra na uvumilivu wa hali ya juu ili kuishi na mtu wa mfano huu. Wanawake wanapaswa wasubiri kwani kama tulivo tanguliza kwa kufanya hayo ujira wake ni zaidi kama ambavo tutaelezea mbeleni katika nakala hii, na uwenda pia kwa kutosubiria hayo, akapata mwengine ambaye ni muovu zaidi zaidi ya huyo mume wake.

Jambo jingine linalopaswa kufahamika ni kuwa, jamii inaundika kwa mjumuiko wa familia mbali mbali, hivyo basi, kwa kuzingatia hayo, ndani ya familia ndo sehemu ambapo twapaswa kujifunza mengi ikiwemo subra na uvumilivu, kwa jinsi ambayo ata tutakapo enda katika jamii, tutakua na uwezo wa kupambana na changamoto wowote unapatikana humo.

Wana ndoa wanapaswa wafahamu kuwa, binadamu sio maasum, ukosea hapa na pale, ndo maumbile ya mwanadamu yalivyo, hivyo yaitajia subra na uvumilivu ili kuishi na mwanadamu mwenzako kwa yale mapungufu na makosa yake utakayo patana nao katika maisha yenu. Na pale kunapopatikana tatizo ni vyema wakaketi wenyewe na wakaitatua kwa kuombana msamaha na kurekebishana, wala sio kila pale panapo patikana tatizo, japo kwa udogo wake, wanakua ni wenye kuifanya kubwa na ata kufikishana kwa wazazi au ata mara nyingine kupelekana adi kwa makadhi.

Hili kufikia hatua ya wawili kuoana, ni kuwa wameamua kuwa, katika maisha yao ya baadae watakua ni wenye kuisha na mwenzake adi pale kifo kitakapo wapata, hivyo basi, wanapaswa wajitahidi na kufikia na kutimiza malengo yao hio, na kupuuzia makosa madogo madogo, na kwa kufanya hivyo kwa hakika ujira wake mbele yake Manani ni kubwa zaidi. Twapaswa tuchukue funzo kutokana na wazazi wetu ambao mbaka sasa wapo pamoja adi katika uzeeni, sababu walipitia subra na yote hayo katika ndoa yao na wakafikia adi hatua hio, hivyo pia nasi tujitahidi katika ndoa zetu tuzifikishe katika hatua hio.

Jambo lingine ambalo ni muhimu ni wana ndoa wanapaswa waheshimu familia na wazazi wa kila mmoja kwa upande huo mwingine, kwani wazazi hao wanageuka kuwa wazazi wapo pia pale mnapoana, kama ambavyo Bwana Mtume (saww) anatuambia;

الآباءُ ثَلاثَةٌ: أبٌ وَلَّدَكَ، و أبٌ زَوَّجَكَ، و أبٌ عَلَّمَكَ»

Baba wako ni watatu; Baba aliekuzaa, baba ambae umeozeshwa na baba aliekusomesha.

Vivo hivo Bwana Mtume(saww) anatuambia kwa kutuonyesha ni ujira kiasi ipi anaepata yule mwenye kusubiria maudhi ya mume wake, anasema (saww);

مَن صَبَرَتْ عَلى سُوءِ خُلُقِ زَوجِها أعطاها مِثلَ (ثَوابِ) آسِيَةَ بنتِ مُزاحِمٍ

Mke atakae subiria tabia mbovu au maudhi ya mume wake, Mwenyezi Mungu atamlipa mema mfano wa alichopewa Bibi asia bint muzaahim,

Kama tunavyo jua halisi aliokuwa akiyaishi bibi asia, ni maudhi mangapi aliyapitia katika ndoa yake na firauni, mwanaume ambae akuna mwanaume muovu mfano wake, lakini bibi asia akayasubiria yote hayo, na kufanywa kuwa ni miongoni mwa wanawake wanne bora hapa duniani, Basi, kwa mwanamke yeyote atakae fanya hayo, akavumilia na kusubiria maudhi yalio ndani ya ndoa yake, mbele ya Mwenyezi Mungu kuna ujira na thawabu tele zamsubiria mwanamke huyo.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Best Topics

Hotest Now

اشترک فی الاجتماعایت

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

للتحمیل اضغط هنا

الرابط المباشر

شارک مع الآخرین :