Follow us in
Follow us in

TUKIO LA MUBAHALA

Kwa jina la mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, mwenye kurehemu

NI NINI MUBAHALA?

Tukio la mubahala halikuwa ni tukio la kujadiliana pekee kama ambavyo imeripotiwa katika historia, bali ni tukio la kubainisha baina ya haki na batili,haki ni ipi na batili ni ipi baina ya uislamu na ukristo.

Tukio hili lilitokea tarehe ishirini na nne mwezi wa dhul hijja mwaka wa 9 hijiria, ambapo wakiristo wa Najran pamoja na viongozi wao walijitokeza hadharani ili kujadiliana na kutaka laana kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa kikundi ambacho kitakua kwenye batili. Ndipo ambapo bwana Mtume saww, aliwatoa watu wake wa wakaribu ili kujadiliana na kikundi hicho cha wakristo, kwa amri ya Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu (swt) katika Quran tukufu anatuambia:

فَمَنۡ حَآجَّكَ فِيهِ مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَكَ مِنَ ٱلۡعِلۡمِ فَقُلۡ تَعَالَوۡاْ نَدۡعُ أَبۡنَآءَنَا وَأَبۡنَآءَكُمۡ وَنِسَآءَنَا وَنِسَآءَكُمۡ وَأَنفُسَنَا وَأَنفُسَكُمۡ ثُمَّ نَبۡتَهِلۡ فَنَجۡعَل لَّعۡنَتَ ٱللَّهِ عَلَى ٱلۡكَٰذِبِينَ

Watakao kuhoji katika haya baada ya kukufikilia ilimu hii waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wake zetu na wake zenu, na sisi wenyewe na nyinyi wenyewe, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.

Asili ya tukio hili ilianza baada ya Mtume saww kuwasiliana na Wakristo wa Najran wanaopatikana Yemen, akiwalingania kuukubali Uislamu au kulipia Jizya. Ujumbe wa Wakristo, ukiongozwa na maaskofu wao, walifika Madina na kujadili mambo ya kidini, wakisisitiza juu ya ukweli wa imani yao kuhusu Yesu kuwa Mungu. Hata hivyo, Mwenyezi Mungu alimteremshia Mtume wake saww amri ya kuwatoa wapendwa wake kama ushahidi wa ukweli wake.

Katika siku hiyo, Mtume Muhammad (saw) hakuja peke yake. Alifuatana na watu waliokuwa wapendwa zaidi kwake; binti yake Fatima Zahra (as), mkwe wake Ali bin Abi Talib (as), na wajukuu zake Hassan na Hussein (as) . Katika Qur’ani, Mwenyezi Mungu amewataja kwa maneno “wana wetu” (Hassan na Hussein), “wanawake wetu” (Fatima), na “nafsi zetu” (Ali), ambapo Imam Ali (as) anachukuliwa kuwa ni “nafsi” ya Mtume (saw) . Hii ni fadhila kubwa ambayo haijawahi kutolewa kwa mtu mwingine yeyote.

Askofu wa Wakristo, Abu Haritha, alipowaona hawa watakatifu wakija kwa ajili ya Mubahala, aliwatisha wenzake na kuwaonya akisema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu, mimi naona nyuso ambazo Mwenyezi Mungu akimuomba aondoe mlima, bila shaka angeliondoa. Usiwahi kufanya Mubahala nao, kwani mkitaka kufanya hivyo, hakika mtaangamia”. Akawaambia, “Muhammad (saw) hangejihadhiri kwa wapendwa wake ikiwa hakuwa na uhakika ya ukweli wake. Ikiwa atatulaani, Mungu hatochelewesha adhabu yake.” Wakristo walikataa kushiriki na badala yake wakakubali kulipa kodi (Jizya).

Mubahala inathibitisha kwamba uongozi wa kiroho na kisiasa wa Uislamu baada ya Mtume saww inamhusu Imam Ali (as) na Ahlul-Bayt kwa kuwa wameunganishwa na Roho ya Mungu. Hii inaonyesha kwamba katika mambo ya dini, mtu anapaswa kurejea kwa Ahlul-Bayt kwa mwongozo. Tukio hili linatumika kama “ushahidi wa dhahabu” wa ukweli wa dhehebu la Shia na Uislamu yenyewe hadi Siku ya Kiyama. Ni ishara kwamba ukweli wa imani unathibitishwa si kwa maneno tu, bali kwa kuhatarisha maisha ya wapendwa katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Best Topics

Hotest Now

اشترک فی الاجتماعایت

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp